Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Liberia inahitaji msaada kuendesha uchaguzi 2011

Liberia inahitaji msaada kuendesha uchaguzi 2011

Liberia inahitaji msaada wa kimataifa wa fedha za ziada ili kuweza kuendesha uchaguzi mkuu mwakani.

Akitoa taarifa kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York leo, mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia Bi Ellen Loj amethibitisha kwamba maandalizi ya uchaguzi wa Rais na wabunge yanaendelea. Ameliambia baraza la usalama kwamba hatua zimepigwa katika kupitisha sheria muhimu na kukusanya fedha. Bi Loj amesisitiza kwamba uchaguzi mkuu wa 2011 ni mtihani muhimu Liberia katika jitihada zake za kupata demokrasia ya kudumu.

(SAUTI YA ELLEN LOJ)

"Ameongeza kuwa ratiba ya uchaguzi ilitangazwa Agosti 27 na daftari la orodha ya wapiga kura litaanza Januari mwakani. Hata hivyo amesema tume ya taifa ya uchaguzi haitoweza kuendesha uchaguzi huo bila msaada wa jumuiya ya kimataifa. Amesema ingawa ahadi nyingi zimetolewa bado juhudi zinahitajika."

Mwakilishi huyo amesema kumekuwa na hatua nyingi nzuri na kwamba miaka saba ya amani na utulivu imeruhusu kuanza kuwa na fikra kuhusu hatma nzuri ya amani ya nchi hiyo