Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yazindua mtandao wa kujifunza maarifa mapya

UNESCO yazindua mtandao wa kujifunza maarifa mapya

Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO linazindua mpango maalumu ambao unajulikana kama mtandao wa maarifa na ubunifu wenye shabaa ya kuwafikia watafiiti na wataalamu wengi duniani ili watekeleze vyema majumu yao.

Mtandao huo ambao uzinduzi wake umekwenda sambamba na siku ya kimataifa ya uelimishaji unakusudia kuwaunganisha wataalamu mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia kwa njia kama kubadilishana taarifa na masuala mengine muhimu.

UNESCO imesema kuwa inatazamia kuelezea zaidi hatua hiyo kwenye kilele cha siku ya kimataifa ya uelimikaji inayofanyika kwenye makao makuu yake Paris, Ufaransa ambako pia kunatazamiwa kuwepo mijadala mbalimbali ikiwemo ile inayozungumzia namna ya kumwezesha mwanamke.

Ama mkuu wa UNESCO Irina Bokova yuko New York ambako atazungumza katika kongamano la kimataifa linaloangazia siku hii yenye kauli mbii isemayo " uelimikaji ni ufungua kwa maendeleo."