UNDP kuandaa mjadala kwa njia ya facebook kuhusu malengo ya milenia
Shirika la mendeleo la umoja wa mataifa kwa mara ya kwanza kabisa linandaa majadiliano ya mtandao ya moja kwa moja kuhusu njia za kukabiliana na umaskini na hatua zinazostahili kuchukuliwa kuafikia maendeleo kabla ya kufanyika kwa mkutano wa umoja wa mataifa kuhusu malengo ya milenia.
Kweye mkutano huo utakaondaliwa kati ya tarehe 20 na 22 mwezi huu mjini New York, viongozi kutoka kila sehemu ya dunia watajadiliana malengo yote manane ya milenia yaliyo na lengo la kupunguza umaskini , njaa, vifo vya watoto , magonjwa , kuwepo kwa maji , usawa wa kijinsi na uharibifu wa mazingira itimiapo mwaka 2015.
Majadiliano yatakayofanywa kupitia kwa mtandao wa Facebook yataongozwa na mkuu wa shirika la UNDP Helen Clark ambapo atajibu maswali yatakayoulizwa kuhusu malengo ya milenia. Kwenye majadiliano hayo shirika la UNDP linatoa fursa kwa watu kutoa maoni yao kuhusu maendeleo na njia za kukabiliana na umaskini na pia kuuliza maswali kuhusu juhudi zinazofanywa na shirika la UNDP kufanikisha malengo ya milenia.