Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN-HABITAT na WWF waafikiana kuilinda mbuga ya Virunga

UN-HABITAT na WWF waafikiana kuilinda mbuga ya Virunga

Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi, UN Habitat na Shirika la Kimataifa la wanyama Pori, WWW, yametia saini mkataba wa pamoja wa kulinda Hifadhi ya Kitaifa ya Virunga iliyoko Mashariki mwa Jamahuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Hatua hii ni ya kwanza kwa mashirka hayo ambayo yana malengo tofauti kushirikiana katika juhudi za pamoja za kulinda Hifadi hiyo ya kitaifa ya wanyama pori ya Virunga, na maeneo mengie yanayohitaji kulindwa. WWF ni shirika kubwa zaidi ulimwenguni linalohusika na ulinzi wa wanyama pori na lilianzishwa mwaka wa 1961.

Na ofisi ya eneo la Mashariki na Kusini mwa Afrika inashughulikia eneo la Kivu ya Kaskazini ambapo hifadhi ya Vurunga inapatikana. Kwa upande wake,shirika la Umoja la Mataifa la Habitat limekuwa likishughulikia na utatuzi wa migogoro ya ardhi mashariki mwa Congo, ikiwemo maeneo yanayopakana na hifadhi ya Virunga, ili kuwasaidia wakimbizi wa ndani kurejea makwao.