UM umekaribisha makubaliano ya orodha ya wapiga kura Ivory Coast
Kwa mujibu wa ujumbe wa ulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika taifa la Magharibi mwa Afrika, makubaliano yaliyoafikiwa kuhusiana na orodha ya mwisho ya wapiga kura nchini Ivory Coast.
Orodha ambayo ilichangia kucheleweshwa kwa muda miezi sita kwa uchaguzi ni hatua muhimu kwa shughuli ya upigaji kura nchini humo. Siku ya Jumatatu mwanachama wa jopo la uwiano, ambalo linawajumuisha Rais Laurent Gbagbo, waziri Mkuu Guillarmo Soro, na wakuu wa vyama viwili , walikubaliana kuhusiana na orodha hiyo.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifda nchini humo, UNOCI inaamini kuwa hatua hii itachagia kuundwa kwa orodha ya mwisho ya wapiga kura na hivyo kufanyika kwa uchaguzi kama ilivyopangwa. Uchaguzi wa Urais Ulipangwa kufanyika mwaka wa 2005 lakini yalihairishwa mara kadha. Lakini uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 31 mwezi wa October.