Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shule za msingi zaidi ya 5000 kupokea vitabu Zimbabwe

Shule za msingi zaidi ya 5000 kupokea vitabu Zimbabwe

Serikali ya muungano ya Zimbabwe, jumuiya ya wahisani wa kimataifa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF leo wamezindua zoezi la kitaifa la kugawqa vitabu mashuleni.

Zoezi hilo litashuhudia shule za msingi 5575 zikipata vifaa vya shule na vitabu , na kila mtoto wa shule ya msingi nchi nzima atapokea mataftari kya masomo yote manne ya lazima. Taarifa zaidi na mwandishi wetu Jason Nyakundi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Utoaji wa vifaa hivyo vya masomo unajiri kufuatia kuzinduliwa kwa mpango wa ufadhili wa elimu ETF mwaka mmoja uliopita ukiwa na lengo la kukusanya vifaa kunua sekta ya elimu. Kwa sasa karibu asilimia 20 ya wanafunzi wa shule za msingi nchini Zimbabawe hawana vitabu kabisa kwa somo la kiingereza , Hesabu pamoja na kwa lugha ya taifa.

Waziri anayehusika na masuala ya elimu , michezo na utamaduni David Coltart anasema kuwa wanafunzi watarejea shuleni na vitabu pamoja na vifaa vingine vya masomo kwa mara ya kwana baada ya miaka tisa akisema kuwa elimu ndiyo nguzo muhimu kwa kuinuka tena kwa taifa la Zimbabwe.