Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msichome Quran:mwakilishi wa UM

Msichome Quran:mwakilishi wa UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Steffan de Mistura amesema kwa niaba ya Umoja wa Mataifa na jumuiya nzima ya kimataifa iliyopo Afghanistan amesema anaelezea hofu yake dhidi ya tangazo la kutaka kukichoma nakala za kitabu kitakatifu cha dini ya Kiislam yaani Quran.

Tanzazo hilo limetolewa nje ya Afghanistan na makundi madogo ya kidini . Demistura amesema suala ya uhuru wa kujieleza lisichanganywe na nia ya kudhalilisha dini au imani ya mamilioni ya watu.

Amesema endapo kitendo hicho cha kuchoma Quran kitatekelezwa basi kitachochea msimamo wa wale wanaopinga amani na maridhiano nchini Afghanistan. Makundi hayo ymeazimia kuzichoma nakala za Quran katika mkesha wa sikukuu ya Eid-ul-Fitr.