Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umeainisha hatua za kulinda raia DRC

UM umeainisha hatua za kulinda raia DRC

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO umechukua hatua kadhaa ili kuimarisha ulinzi wa raia mashariki mwa nchi hiyo.

Hatua hiyo imefuatia matukio ya hivi karibuni ya ubakaji wa idadi kuwa ya watu. Akizungumza kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana jioni mwakilishi wa Katibu Mkuu katika idara ya operesheni za kulinda amani Atul Khare amesema kuhakikisha udhibiti wa serikali katika maeneo yaliyoathirika na vita kutasaidia kumaliza hali ya kutochukuliwa sheria na ghasia katika maeneo hayo. Mwandishi wetu George Njogopa anayo maelezo.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA,)

Atul Khare amesema hakuna njia ya mkato inayoweza kuleta utengamao wa kudumu kwenye eneo hilo liliharibiwa vibaya na machafuko ya vita, mbali ya kuanza kuweka mamlaka za dola ili kudhibiti vitendo hivyo vya kihalifu.

Akielezea kuhusiana na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na kikosi maalumu cha MONUSCO, amedai kuwa tayari kikosi hicho kimeendesha operesheni maalumu hasa katika eneo la Kivu ya Kaskazini ambako vitendo vya ubakaji viliripotiwa kwa wingi kwa shabaya ya kuwaongezea ulinzi wananchi.  Aidha Atul Khare amefahamisha kuwa, juhudi za kuimarisha usalama kwenye eneo hilo zimeanza kuungwa mkono na wananchi