Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Angola na DR Congo zakumbwa tena na polio

Angola na DR Congo zakumbwa tena na polio

Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanakabiliwa na mlupuko mpya wa virusi vya polio type 1.

Nchini Angola ambako mlipuko ulizuka mwezi April 2007, mwaka huu maambukizi yamesambaa kwenye majimbo mengi ya nchi hiyo kiwemo nchi. Maelezo zaidi na mwandishi wetu Jason Nyakundi.

(RIPOTI NA  JASON NYAKUNDI)

Ugonjwa huo unaotajwa kuwa aina ya WPV1 sasa umesambaa hadi mikoa ya Bie, Bengo, Huambo, Lunda Norte, Lunda Sul na Uige nchini Angola na pia kwenye maeneo ya karibu ya Jamhuri ya kidemokrasi a Congo. Kwa sasa enea la afrika ya kati linatajwa kuwa lililo kwenye hatari ya mardhi ya Polio huku ugonjwa huo ukitajwa kusambaa zaidi nchini Angola.

Hali hii sasa inatajwa kuwa kizingiti katika mpango wa kimataifa wa mwaka 2010 -2012 wa kungamiza ugonjwa wa Polio. Hata hivyo asilimi 99 ya ugonjwa huo umeangamizwa nchini Nigeria ikilinganishwa na mwaka uliopita wakati ambapo hakuna visa vyovyote vya ugonjwa huo vimeripotiwa maeneo la Afrika magharibi tangu mwezi Mei mwaka huu.