Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umebainisha uwezo wa umuhimu wa uwezeshaji katika kuinua kiwango cha kujua kusoma na kuandika kwa wanawake

UM umebainisha uwezo wa umuhimu wa uwezeshaji katika kuinua kiwango cha kujua kusoma na kuandika kwa wanawake

Leo ni siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika. Katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kujua kusoma na kuandika kunabadili maisha ya wanawake,familia zao, jumuiya zao na jamii zao.

Ameongeza kuwa wanawake waliosoma wananafasi kubwa ya kuwapeleka watoto wao shuleni na hususani kuhakikisha motto wa kike anapata elimu. Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO likiadhimisha siku hii linazindua mtandao wa taaluma mpya na uzinduzi wa kujua kusoma na kuandika KINL.

Mtandao huo utawasaidia watafiti wanazuoni duniani kote kuwasiliana na kubadilishana taarifa na uzoefu. Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York ambapo mkurugenzi wa UNESCO Irina Bokova na mke wa Rais wa zamani wa Marekani Laura W. Bush wamezungumzia mada ya kujua kusoma na kuandika ni msingi wa maendeleo. Bokova amesema bado wanawake wengi hawajui kusoma na kuandika

(SAUTI IRINA BOKOVA )

Anasema mpaka sasa bado mtu mmoja kati ya sita hajui kusoma na kuandika duniani kote, wengi wao ni wanawake, na katika baadhi ya nchi chini ya asilimia 50 ya wanawake ndio wanajua kusoma na kuandika ikimaanisha wengi bado hawajui kusoma na kuandika, na katika hali hii haiwezekani kumaliza mzunguko wa umasikini na kutokuwa na usawa.