Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kusaidia wakimbizi wa Rwanda wanaorejea nyumbani

IOM kusaidia wakimbizi wa Rwanda wanaorejea nyumbani

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa kushirikiana na wizara ya Rwanda ya udhibiti wa majanga na masuala ya wakimbizi MIDIMAR wamezindua mradi wa kutoa fursa za kijamii na kiuchumi kwa wakimbizi wa Rwanda wanaorejea nyumbani na makundi mengine yasiyojiweza.

Mradi huo unasaidia makundi mbalimbali ya wahitaji katika majimbo ya Kusini na magharibi mwa Rwanda baada ya kutathimini iliyofanywa na IOM na kubaini mahitaji muhimu. Baadhi ya masuala yaliyoangaliwa ni pamoja na uhakiki wa masuala ya ujuzi, mahitaji ya mafunzo, tathimini ya uwezo wa maendeleo na utekelezaji wa mikakati iliyowekwa na serikali ya Rwanda.

Lengo lingine la mradi huo ni kuimarisha uwezo wa serikali ya Rwanda kukabili idadi ya wakimbizi wanaorejea nyumbani. Inakadiriwa kuwa wakimbizi 72,000 wa Rwanda wako nje na wengi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku wengine 20,000 wamerejea nyumbani kwa mwaka 2009 pekee.