Balozi mwema wa UNHCR anazuru Pakistan kujinea hali halisi

Balozi mwema wa UNHCR anazuru Pakistan kujinea hali halisi

Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Angelina Jolie yuko nchini Pakistan kujionea athari za mafuriko kwa mamilioni ya watu ambao bado wanahitaji msaada.

Leo na kesho Jolie anazuru majimbo yaliyoathirika sana na mafuriko, katika ziara hiyo anakutana na waathirika na pia watu wanaohusika na shughuli za misaada. Mcheza filamu huyo maarufu aliyejishindia tuzo, mara ya mwisho alizuru Pakistan mwaka 2005 baada ya tetemeko kubwa la ardhi kaskazini mwa nchi hiyo.

Mamilioni ya watu wameathirika na mafuriko hayo ya Pakistan na UNHCR hadi sasa imetoa msaada kwa watu takribani 750,000.