Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia za masuala ya chakula Msumbiji zilitarajiwa:UM

Ghasia za masuala ya chakula Msumbiji zilitarajiwa:UM

Kufuatia ghasia za matatizo ya chakula nchini Msumbiji ambazo zimesababisha vifo na watu wengi kujeruhiwa, na pia hali hii kubainika katika nchi nyingine, mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya chakula Olivier De Schutter amezitaka serikali na jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na msukosuko wa soko la kimataifa la chakula.

Bwana De Schutter  Amesema hikubaliki kuiacha hali hii iendelee.

(SAUTI YA DE SCHUTTER)

Bwana De Schutter ameongeza kuwa tunajua wapi mfumo wa chakula unaposhindwa, tunajua ni hatua gain zinapaswa kuchukuliwa, lakini ukosefu wa ari ya kisiasa na kutozingatia dharura kumesababisha kuchelewa kuchukuliwa hatua.

Ameutaka mkutano wa dharura ulioitishwa na Umoja wa Mataifa na shirika la chakula na kilimo FAO utakaofanyika Septemba 24 mjini Roma kuchukua hatua zaidi ya maneno, na uandae mipango ya uhifadhi wa chakula na amewatolea wito wahisani kuongeza juhudi za kuzisadia nchi zenye upungufu wa chakula.