Kuwekeza kwa watoto masikini kabisa kutasaidia kuokoa maisha ya mamilioni:UM

Kuwekeza kwa watoto masikini kabisa kutasaidia kuokoa maisha ya mamilioni:UM

Utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF umebaini kwamba jumuiya ya kimataifa inaweza kuokoa maisha ya mamilioni ya watoto kwa kuwekeza kwanza kwa watoto na jamii sisizojiweza.

UNICEF inasema matazamo huo pia utasaidia kushughulikia kasoro zinazoongezeka na kuathiri mchakato wa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia(MDG'S). Matokeo ya utafiti huo yanawasilishwa katika matoleo mawili. La kwanza ni "Kupunguza pengo ili kufikia malengo na hatua kwa watoto na la pili ni "Kufikia malengo ya maendeleo ya milenia kwa usawa".

Kwa mujibu wa utafiti huo wakati hatua kubwa zimepigwa kimataifa kufikia malengo hayo bado hatua zaidi zinahitajika katika miaka mitano ijayo. Utafiti huo umefanyika kwa kushauriana na wataalamu mbalimbali wa nje ambao wameelezea matokeo yake kuwa ni ya muhimu na ya kushangaza.