Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asisitiza kulindwa kwa jamii maskini hata kama kuna msukosuko wa kuichumi duniani

Ban asisitiza kulindwa kwa jamii maskini hata kama kuna msukosuko wa kuichumi duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa wito kwa nchi tajiri kutozisahau zile maskini na kuzitaka kujitolea kuzisadia nchi hizo ili kuziwezesha kukabiliana na umaskini ili ziweze kupiga hatua za kimaendeleo.

Akiongoea kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu msukosuko wa kiuchumi na malengo ya milenia katika eneo la Alpbach nchini Austria Ban amezitaka nchi ambazo utajiri wao ulistahimili msukosuko wa kiuchumi kuzidaia nchini maskini kupambana na tatizo la umasikini.

Ban amesema kuwa kutotabirika kwa hali ya kiuchumi katika siku zijazo hakitakuwa kisingizio kwa kutotimizwa kwa melengo ya milenia akisema kuwa ushirikiano wa dunia yote ndiyo nguzo ya kufanikisha malengo ya milenia.

Ban amesema kuwa ni lazima kubuniwa nafasi za ajira na kuwekeza zaidi upatikanaji wa maji safi na kuwepo kwa nishati safi kwa manufaa ya maendeleo ya kiteknolojia na kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa.