Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali mpya ya Burundi imeapishwa

Serikali mpya ya Burundi imeapishwa

Huko Burundi, Rais wa nchi hiyo Pierre NKURUNZIZA amekula kiapo kuendelea kuongoza taifa hilo katika muhula mungine wa miaka mitano baada ya kuchaguliwa kwenye uchaguzi uliosusiwa na vyama vya upinzani.

Rais NKURUNZIZA ameteuwa baraza jipya la mawaziri ambapo sehemu kubwa ya mawaziri wamesalia kwenye nyadhifa zao awali. Ametumia fursa hiyo kutangaza vita dhidi ya tabia ilikithiri ya ufisadi na ufujaji wa mali ya umma .

Kutoka Bujumbura ,Muandishi wetu Ramadhani KIBUGA ametutumia taarifa hii.