Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maafisa wa UM waeleza wasi wasi kutokana na kuzorota haki za binadamu DRC

Maafisa wa UM waeleza wasi wasi kutokana na kuzorota haki za binadamu DRC

Wakuu wa Umoja wa Mataifa wameeleza wasi wasi kutokana na kuzorota kwa hali ya haki za binadamu huko mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

mwishoni mwa mwezi uliopita mwanaharakati wa haki za binadamu alitekwa nyara na wanajeshi na kuachiliwa huru baadae, na kusababisha kutolewa wito wa hatua kuchukuliwa haraka kukabiliana na hali hiyo. Zayana jabir ana maelezo zaidi juu ya hali hiyo katika makala yetu maalum.