Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yazindua mtandao mpya kuadhimisha siku ya kujua kuandika na kusoma Duniani

UNESCO yazindua mtandao mpya kuadhimisha siku ya kujua kuandika na kusoma Duniani

Idara ya Elimu na Sayansi ya UM itazindua mtandao mpya wa elimu na uvumbuzi KNL ambao utawawezesha watafiti na watalamu wa kazi kote duniani kuwasiliana na kubadilishana habari na ujuzi wao.

Kuzinduliwa kwa mtandao huo itakua kilele cha sherehe za siku ya

kimataifa ya kujua kusoma na kuandika duniani hapo Septemba 8 katika makao makuu ya UNESCO huko Paris. Kauli mbinu ya mwaka huu ni "kujua na kyusona na kuwawezesha wanawake,"

Mkurugenzi mkuu wa UNESCO Bi Irina Bokova atatoa hotuba kuu mjini New York kwenye mkutano wa kimataifa juu ya Kusoma na kuandika kama msingi muhimu kwajili ya maendeleo. Na kwenye makao makuu ya Paris sherehe za kutoa tunzo ya mwaka ya kusoma na kuandika ya UNESCO, zitafanyika ambapo miradi ya huko Cape Verde na Ujerumani zitapokea tunzo hiyo ya juu.