Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti mpya ya UNRISD juu ya kupambana na umaskini

Ripoti mpya ya UNRISD juu ya kupambana na umaskini

Taasisi ya Utafiti kwa ajili ya maendeleo ya kijamii ya UM, UNRISD imeonya kwamba muelekeo wa hivi sasa wa kupambana na umaskini au kutenganisha umaskini kutoka utaratibu mpana wa ukuwaji wa kiuchumi na maendeleo umepangwa vibaya.

Ripoti mpya ya UNRISD juu ya kupambana na umaskini na ukosefu wa usawa iliyozinduliwa Geneva leo inachunguza sababu, mwenendo wa umaskini na kwanini unaendelea kua sugu, pamoja na kuchambua mambo yanayofanya kazi na yasiyofanya kazi katika sera za kimataifa.

Mratibu wa utafiti wa UNRISD Yusuf Bangura ambae aliongoza kuandika ripoti hiyo anadai ukosefu wa mafanikio unatokana na kupuzi sababu msingi za umaskini.

"Tunatoa hoja kwamba umaskini unahusina kwa karibu na aina nyenginezo za ukosefu wa usawa, kama vile tabak, jinsia na ukabila, na hali hii ya kutokua na usawa mara nyingi hukwamisha maendeleo. Kwa mfano inasababisha hali kuwa ngumu kuhusisha watu maskini katika utaratibu wa ukuiwaji"

Anasema katika nchi nyingi ukosefu wa usawa katika mapato na utajiri umeongezeka na ukosefu wa usawa unazidi kwa misingi ya kikabila na jinsia.

Ripoti inamulika matokeo kutoka nchi ambazo zimefanikiwa katika kuimarisha sana maisha ya sehemu kubwa ya raia wake.