Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Balozi mfadhili wa UNEP ni kati ya wasanii wanaoendesha kampeni dhihi ya umaskini

Balozi mfadhili wa UNEP ni kati ya wasanii wanaoendesha kampeni dhihi ya umaskini

Mcheza filamu na balozi mfadhili wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Don Cheadle ni kati ya wasanii walioteuliwa na Umoja wa Mataifa kuongoza kampeni dhidi ya umaskini kote duniani na pia kushinikiza kutimizwa kwa malengo ya milenia ikiwa imesalia miaka mitano kabla ya mwaka 2015 ambao ni mwaka wa kutimizwa kwa malengo hayo .

Malengo yote manane ambayo waliafikia viongozi duniani kwenye mkutano mkubwa mwaka 2000 kwa sasa umoja wa mataifa unafanya mikakati ya kufanikishwa kutimizwa kwa malengo hayo. Kwa sasa Cheadle anatoa hamasisho kuhusu mazingira kwa mamilioni ya watu kote dunini ikiwa ni moja ya njia ya kuliangazia lengo nambari saba linalohusika na utunzi wa mazingira kama moja ya melengo hayo. Sasa kama balozi wa malengo ya milienia balozi huyo ataongoza kampeni kwenye masuala kadha yanayohusiana na malengo hayo yakiwemo ya kuangamiza umaskini njaa na magonjwa. Mabalozi wa malengo ya milenia waliteuliwa kutoka kwa kundi la mabalozi wa umoja wa mataifa wakiwemo wanasoka , wanamitindo na wanamiziki. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amewashukuru mabalozi hao kwa kushiriki kufanikisha melengo hayo.