Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada zaidi wahitajika kwa waathiriwa wa mafuriko Pakisan:Angelina Jolie

Msaada zaidi wahitajika kwa waathiriwa wa mafuriko Pakisan:Angelina Jolie

Balozi mfadhili wa Idara ya kuwahudumia wakimbizi ya Umoja wa Mataifa Angelina Jolie, ametoa wito wa kuwepo na ungaji mkono mkubwa zaidi kutoka kwa watu wote duniani kwa ajili ya juhudi za kuwapatia huduma za dharura mamilioni ya watu ambao maisha yao yameharibiwa kabisa kutokana na mafuriko makubwa huko Pakistan.

Katika ujumbe wa video ulotolewa leo, mcheza filamu huyo alizungumzia kiwango cha maafa nchini humo:

(SAUTI YA ANGELINA JOLIE)

Angelina Jolie ametoa dola 100,000 kwa UNHCR kusaidia kukabiliana na janga hili la mafuriko.

Wakati huo huo mwakilishi wa UNHCR huko Pakistan, Bw Mengesha Kebede ameeleza wasi wasi wake kutokana na kuzorota kwa hali ya kibinadamu katika jimbo la Balochistan, magharibi ya Pakistan, na kutoa wito wa kuongezwa kwa kazi za huduma za dharura. Bw Kebede alisema hali ya mafuriko katika jimbo hilo la milima kwa sehemu kubwa haikutiliwa maanani wakati macho ya dunia yalikua yanaelekezwa katika mafuriko ya Mto Indus kuelekea upande wa kusini.

Bw Kebede alionya kwamba hali huko Balochistan imefikia kiwango cha maafa ya kibinadamu na ikiwa hakuna hatua zitachukuliwa basi huwenda hali ikageuka na kua janga kuu la kibinadamu nchini Pakistan. UNHCR imekua ikitoa hema na misaada mengine ya makazi huko Balochistan na inamipango ya kuimarisha huduma zake huko.