Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM anasema lazima Mazungumzo ya Mashariki ya Kati yatanzuwe masuala msingi

KM anasema lazima Mazungumzo ya Mashariki ya Kati yatanzuwe masuala msingi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anasema ni lazima mazungumzo ya Mashariki ya Kati yawe ya kweli na yatanzuwe masuala msingi kwa ajili ya kupatikana amani ya kudumu huko Mashariki ya Kati.

Bw Ban alikua anazungumza huko Liechtenstein kabla ya kuanza mazungumzo ya Washington kati ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na rais wa Palestina Mahmoud Abbas hii leo. Katibu Mkuu anasema amefurahishwa na mazungumzo ya moja kwa moja kati ya viongozi hao wawili na yuko tayari na ana nia ya kurahisisha maendeleo ya mazungumzo haya ya amani.

(SAUTI YA BAN)

Bw Ban alisema hii ni sehemu moja tu ya juhudi zinazoendelea kufanyiwa kazi kwa pamoja na washirika wa pande zote.