Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waonya kuwa watu wanaanguka wameongezeka na kuzidisha wasiwasi kwa afya za wengi

UM waonya kuwa watu wanaanguka wameongezeka na kuzidisha wasiwasi kwa afya za wengi

Takwimu zilizotolewa na Shirika la afya ulimwenguni WHO zimeonyea kuwa, hali ya kuanguka ni janga jingine ambalo linachangia pakubwa kuzorotesha afya ya binadamu kwani katika kipindi cha mwaka mmoja kuna wastani wa watu 424,000 wameanguka duniani kote jambo ambalo linakaribisha majanga mengine kwenye maisha yao.

Watu wenye umri mkubwa, ndiyo wapo hatarini zaidi kwani wananafasi ndogo ya kupona iwapo wanaanguka ni hii kutokana na baadhi ya viongo vyao kuanza kupoteza nguvu halisi ya kustahimili mitetemo na mishtuko.