Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa UM atembelea eneo lililokumbwa na vitendo vya ubakaji DRC

Afisa wa UM atembelea eneo lililokumbwa na vitendo vya ubakaji DRC

Afisa wa Umoja wa Mataifa aliyeko ziarani nchini Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo kufuatilia vitendo vya ubakaji ambavyo vinadaiwa kufanywa na makundi ya kihalifu kwa mamia ya raia amewasili katika eneo la mashariki kwa nchi hiyo ambako ndiko vitendo hivyo vya ubakaji vilifanyika.

Atul Khare ambaye ni msaidizi wa Katibu Mkuu anayehusika na ufuatiliaji wa amani, anatazamiwa kutembelea miji ya Goma,Kirumba, Kibua, Bukavu na Uvira ambako vitendo vya ubakaji vinaarifiwa kuripotiwa kwa wingi.

Aidha kabla ya kuelekea kwenye eneo hilo la Mashariki wa Congo Afisa huyo waUmoja wa Mataifa alikutana na kufanya mazungumzo na maafisa kadhaa wa serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje,Naibu Waziri Mkuu na mshauri wa usalama kwa rais. Pia katika mji huo wa Kishasa afisa huyo alipata fursa ya kukutana na wawakilishi wa mashirika ya kirai.

Raia zaidi ya 154 ambao ni wananchi wa kawaida walibakwa katika kipindi cha kuanzia july 30 hadi august 2 nchini Congo.