Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WIPO yapongeza Afrika kwa kuwa na chombo cha kutetea utamaduni kale wake

WIPO yapongeza Afrika kwa kuwa na chombo cha kutetea utamaduni kale wake

Shirika la Umoja wa Mataifa lililo na jukumu la kulinda na kuhifadhi mali kale, umeelezea kuridhishwa kwake na hatua ya hivi karibuni ya nchi za Afrika kupitisha chombo kipya kitakachowajibika na dhamana ya kulinda utamaduni wa kale ambao unajumuisha pia urithi wa elimu.

Chombo hicho kipya kilichoridhiwa hivi karibuni huko Swakopmund, Namibia, pamoja na mambo mengine kinashaba ya kuhakikisha kwamba utamaduni wa kiafrika unahifadhiwa kwa ajili ya kuwaletea maendeleo waafrika wenyewe.

Mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa anayehusika na uhifadhi wa mali kale WIPO, Francis Gurry, amekaribisha hatua hiyo ikisema kuwa inafungua historia mpya ya uhifadhi wa utamaduni wa kiafrika