Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano juu ya mkataba wa haki za walemavu unazingatia athari za migogoro kwa watu wenye ulemavu

Mkutano juu ya mkataba wa haki za walemavu unazingatia athari za migogoro kwa watu wenye ulemavu

Kikao cha tatu cha mkataba wa haki za watu wenye ulemavu umeanza mjini New York Hii leo na utazingatia zaidi juu ya haki za watu wenye ulemavu katika maeneo ya hatari na majanga.

Mkuu wa afisi ya mkataba wa haki za  walemavu Akiko Ito alisema matokeo ya ulemavu huongezeka wakati wa migogoro na majanga na hivyo walemavu hukabiliwa na hatari zaidi wakati wa hali ya dharura.

Mkutano huo wa siku tatu ulotayarisha kwa ushirikiano na muungano wa kimataifa walemavu, unajadili juu ya masuala hayo kutokana na kuongezeka hivi karibuni kwa migogoro ya utumiaji silaha na majanga asili kama mtetemeko wa ardhi wa Haiti na mafuriko huko Pakistan.

Wajumbe kwenye mkutano watajadili pia juu ya njia za kuhakikisha kwamba walemavu wanahusishwa kwa kikamilifu katika maisha ya jamii zao na kwamba mahitaji yao ya masomo yanazingatiwa kwa dhati.

Mataifa 146 yalitia saini mkataba huo na hadi sasa ni mataifa 90 yaliyokwisha idhinisha.