Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha hatua ya Palestina na Israel kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana

UM wakaribisha hatua ya Palestina na Israel kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana

Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa inayoshughulia haki za Palestina imekaribisha kwa furaha hatua ya pande mbili Palestina na Israel ya kuafiki kuendelea tena na majadiliano yanayokusudia kumaliza mzozo.

Hii ni hatua muhimu inayokaribisha hali ya maelewano na ishara kwamba ni mwanzo wa kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa mzozo huu wa mashariki ya kati, imesema taarifa ya Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa inayohusika na Palestina.

Hii ni mara ya kwanza kwa pande hizi mbili kurejea tena mezani na kuwa na mazungumo ya ana kwa ana, kwani mara ya mwisho mazungumzo kama haya yalifanyika mwaka 2008.