Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi dhidhi ya walinda amani nchini Somalia

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi dhidhi ya walinda amani nchini Somalia

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulizi lililolenga ikulu ya rais lililowaua walinda amani wanne kutoka Uganda wanaohudumu kwenye kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika nchini Somalia.

Ikilu ya rais ilishambuliwa kwa mabomu mjini Mogadishu wakati wanamgamo wa kislamu wanapoendelea kuipiga vita seriklai ya mpito nchini Somalia inayoungwa mkono na kikosi ya muungano wa afrika AMISON.

Kwenye ripoti kwa vyombo vya habari wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kile limekitaja kuwa ghasia dhidi ya raia. Wanachama hao 15 pia wamelaani kuongozeka kwa mapigano nchini Somalia na kusema kuwa wanaiunga mkono serikali ya mpito katika harakati zake za kuleta amani na usalama kupitia kwa mpango wa amani wa Djibouti. Aidha wanachama hao wamezipongeza serikali za Uganda na Burundi kwa kuchangia kikosi cha wanajeshi wanaolinda amani nchini Somalia.