UNIFEM kuwatayarisha wagombea wanawake kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka huu

31 Agosti 2010

Idara ya Maendeleo kwajili ya Wanawake ya Umoja wa Mataifa UNIFEM, inaanda warsha mwezi mzima wa Septemba, katika wilaya saba za uchaguzi nchini Tanzania ili kuimarisha mikakati ya uchaguzi ya wagombea wanawake, kabla ya uchaguzi mkuu wa October.

Mafunzo hayo yanalengo la kuwawezesha wagombea wanawake kwa kuimarisha ujuzi wao wa kuzungumza hadharani, kuwasiliana na vyombo vya habari, kupanga kampeni zao, kuhamasisha pamoja na namna ya kujitetea. Wagombea watapata mafunzo pia juu ya wanawake katika siasa za Tanzania, masuala ya hivi sasa yanayoambatana na uchaguzi, jukumu la Bunge la Taifa, mabunge ya wilaya na mitaa na umuhimu wa sheria, kanuni na masharti ya uchaguzi.

Naibu Mkurugenzi wa UNIFEM kwajili ya maendeleo ya kikanda huko Pembe ya Afrika na Mashariki Ni Sha, alisema ni lazima kwa wanawake na wanaume kuungana kuhamasisha uwakilishaji wa sawa, kushiriki na uwongozi wa wanawake katika utaratibu wa kisiasa.

Katika uchaguzi mkuu uliyopita huko Tanzania 2005, ni wanawake 17 waloshiriki kugombania viti 232 vya bunge.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud