UNICEF yapongeza kuundwa kitengo cha kuwalinda watoto Sudan ya Kusini

31 Agosti 2010

Idara ya Watoto ya Umoja wa Mataifa UNICEF imeipongeza serikali ya Sudan ya Kusini kuundwa na kuzinduliwa kitengo cha kulinda watoto ndani ya Jeshi la Ukombozi wa Sudan ya Kusini SPLA, ikielezea kwamba hiyo ni hatua ya kihistoria kwajili ya haki za watoto nchini humo.

Kuundwa kwa kitengo hicho kunafuatia mpango wa hatua ulotiwa saini na SPLA ikiahidi kuwachili watoto wote katika viwango vyote ifikapo Novemba 2010 na kukomesha kuwatumia watoto kama wanajeshi kote Kusini mwa Sudan.

Akizungumza wakati wa sherehe za kuzindua kitengo hicho, mwakilishi wa UNICEF huko Sudan ya Kusini Catherine Mbengue, alisema hatua hiyo ni ushahidi wa dhamira ya serikali ya Sudan ya Kuisni na SPLA kuharakisha kubuniwa mazingira ambayo haki za watoto wote zina heshimiwa.

Kitengo cha kulinda watoto kinajukumu la kuhakikisha kwamba hakuna watoto katika viwango vyote vya SPLA. UNICEF itatoa msaada wa kifedha na kiufundi kuendeshwa kampeni ya kuhamasisha maafisa wa SPLA.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter