Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unalaani kuuliwa wagombea wawili na wafanyakazi wa kampeni Afghanistan

UM unalaani kuuliwa wagombea wawili na wafanyakazi wa kampeni Afghanistan

Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Afghanistan UNAMA imelaani kuuliwa kwa wagombea wanne wa uchaguzi wa bunge katika jimbo la magharibi la Herat huko Afghanistan pamoja na mauwaji ya watu watano wanaosaidia katika kampeni za uchaguzi za mgombea mmoja mwanamke katika jimbo hilo hilo.

Wanaohusika na mauwaji hayo hadi hivi sasa hawajulikani. UNAMA imepeleka risala za rambi rambi kwa familia za walopoteza maisha yao na kutaka walohusika na mauwaji hayo kufikishwa mahakamani. Ofisi hiyo imeeleza mauwaji hayo kua ni vitisho vya ghasia dhidi ya wagombea uchaguzi na wafuasi wao.

Katika taarifa yake UNAMA inatoa wito kwa vikosi vya usalama vya Afghanistan kua katika hali ya juu ya tahadhari katika wiki kabla ya uchaguzui wa bunge utakaofanyika Septemba 18