Skip to main content

Mahakama ya ICC yaueleza Umoja wa Mataifa kuhusu ziara ya rais wa Sudan nchini Kenya aliyepewa waranti wa kukamatawa na mahakama hiyo

Mahakama ya ICC yaueleza Umoja wa Mataifa kuhusu ziara ya rais wa Sudan nchini Kenya aliyepewa waranti wa kukamatawa na mahakama hiyo

Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu ICC imelieleza baraza la usalama la umoja wa mataifa kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir anayetafutwa na mahakama hiyo kujibu mashtaka ya mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu alizuru Kenya ambayo ni mwanachama wa mahakama hiyo nchi inayostahii kumkamata na raia Bashir.

Mwezi uliopita mahakama ya ICC ilitangaza waranti wa pili wa kutaka kukamatwa kwa rais Bashir kuhusiana na uhalifu aliotekeleza katika jimbo linalokabiliwa na mzozo la Darfur kusini mwa Sudan. Mwezi machi mwaka 2009 rais Omar al-Bashir alikuwa rais wa kwanza aliye mamlakani kupewa waranti wa kukamatwa na mahakamaya ICC baada ya kupatikana na makosa ya kuhusika kwenye uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.