Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu kuizuru Peru

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu kuizuru Peru

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kulinda haki za binadamu anatarajiwa kufanya ziara rasmi ya juma moja nchini Peru kwa mwaliko wa serikali.

Ziara hiyo ya Martin Scheinin itango'oa nanga tarehe mosi hadi nane mwezi septemba mwaka huu ambapo anatarajiwa kufanya mikutano na viongozi wa serikali wakiwemo mawaziri wa serikali na pia mwanasheria mkuu. Scheinin pia majadiliano na idara ya mahakama , bunge na tume kadha zinazolinda na pia kutetea haki za binadamu. Atakutana na waakilishi wa jamii ya kimataifa, waathiriwa na mashambulkizi ya kigaidi , mawakili, wasomi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikai. Katika ziara yake mtaalamu huyo atazuru mji wa Lima na maeneo ya Ayacucho na Cusco na maeneo wanamozuiliwa washukiwa wa ugaidi ambapo pia atawahoji waliohukumiwa kwa kuhusika kenye ugaidi kabla ya kuwahutubia waandishi wa habari tarehe nane mezi ujao mjini Lima atakapokamilisha ziara hiyo.