Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wa Kenya wazungumzia changamoto zinazowakabili

Vijana wa Kenya wazungumzia changamoto zinazowakabili

Makala yetu ya wiki hii inamulika juu ya Mkutano wa kimataifa wa vijana unaofanyika huko Leon Mexico. Wajumbe kutoka zaidi ya serikali mia moja pamoja na mashirika yasio ya kiserikali, Umoja wa Mataifa na vijana wanahudhuria mkutano huo na kujadili juu ya masuala mbali mbali yaliyomuhimu kwa vijana

kuanzia elimu, afya, ajira, umaskini, siasa na uhamiaji. Robo moja ya wakazi wote duniani ni vijana chini ya miaka 24 ambapo tisa kati ya vijana kumi wanaishi katika nchi zinazoendelea. Mwandishi wetu kutoka Nairobi Jason Nyakundi ametayrisha makala juu ya matumaini na maoni ya vijana huko Kenya kuambatana na mkutano huo wa Mexico .

(PKG JASON NYAKUNDI)

Shukrani Jason Nyakundi kwakutukamilishia makala hii ambayo pia inapatikana moja kwa moja kwenye tovuti yetu kupitia www.unmultimedia.org ,kwenye twitter na facebook. Imekujia kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya Umoja wa Mataifa. Mini ni Alice Wairimu Kariuki Kwaheri kutoka New York