Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wahamishwa katika maeneo ya usalama huko CAR kwa hofu ya mashambulio ya LRA

Wakimbizi wahamishwa katika maeneo ya usalama huko CAR kwa hofu ya mashambulio ya LRA

Idara ya kuwahudumia wakimbizi ya Umoja wa Mataifa UNHCR imeanza kuwahamisha kiasi ya wakimbizi 1 500 wa Jamhuri ya Afrika ya Kati walotawanyika kwenye mpaka kati ya Congo na Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuwapeleka katika kambi mpya ya wakimbizi km 70 ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

UNHCR inasema lengo la kuwahamisha ni kuwaweka katika hali ya usalama zaidi ili kupunguza uwezekano wa mashambulio mapya ya LRA. Zaidi ya kuwalinda na kuwapatia hifadhi kambi hiyo mpya ina maji masafi na huduma nzuri zaidi za dharura.