Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu Ban awapongeza Wakenya kwa katiba mpya

Katibu Mkuu Ban awapongeza Wakenya kwa katiba mpya

Rais Mwasi kibaki wa Kenya aliidhinisha katiba mpya wakati wa sherehe za kihistoria zilizofanyika Ijumaa asubuhi kwenye uwanja wa Uhuru mjini Nairobi na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa kutoka mataifa jirani, wapatanishi wa mzozo wa Kenya pamoja na maelfu ya wananchi.

Kufuatia kutiwa saini katiba hiyo mpya, Rais Kibaki na wajumbe wa serikali yake walikula upya kiapu chini ya katiba hiyo mpya.

Kenya inapata katiba mpya kwa mara ya kwanza miaka 47 tangu kujinyakulia uhuru kutoka kwa ukoloni wa Uingereza, waziri mkuu Raila Odinga akipongeza ufanisi huu alisema.

Sasa ni juu ya viongozi wa Kenya kuhakikisha katiba inatekelezwa namna ipasavyo na kwa matumaini ya wakenya.

Umoja wa Mataifa uliwapongeza wa-Kenya walipokamilisha kura ya maoni kwa amani na kupitisha katiba hiyo mpya hapo Agosti 6 mwaka huu na Katibu mkuu Ban K-moon katika ujumbe wake alisema hiyo katiba ni hatua muhimu katika kukabiliana na changamoto za muda mrefu za nchi hiyo.