Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UN juu ya Somalia anatoa wito wa kampain ya kitaifa kuzuia umwagikaji damu zaidi

Mtaalamu wa UN juu ya Somalia anatoa wito wa kampain ya kitaifa kuzuia umwagikaji damu zaidi

Mtaalmu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na hali ya haki za binadam nchini Somalia Dk Shamsul Bari ametoa wito kwa wa-Somali wote kutoka kila tabaka ya jamii kulaani vikali kabisa shambulio la Agosti 24 dhidi ya hoteli Muna mjini Mogadishu lililosababisha vifo vya watu 33.

Dk Bari alisema wasomali wote wa ndani na nje ya nchi wanahamu kuona amani imerudi na haijabidi wanyimwe haki hiyo. Alisema shambulio hilo la kikatili kwa mara nyingine tena linaonesha kwamba wenye siasa kali hawajali chechote katika jaribio lao kunyakua madaraka kwa nguvu.

Wabunge wanne wa serikali ya mpito waliuwawa kwenye shambulio hilo, maafisa watano wa usalama pamoja na raia wasio na hatia.

Mtaalamu huru alitoa wito kwa wasomali pia kusaidia kuzuia kutokea tena aina yeyote ya ukatili wa namna hiyo na kusaidia katika kuwafikisha mahakamani walohusika.

Alitoa wito kwa jumuia ya kimataifa kutafakari upya na kurudia tena ahadi zao za kuwapatia ulinzi raia na uwezo wa kupata msaada wa dharura ikiwa ni kipau mbele cha juu huko Somalia.