Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN unayahimiza mataifa yote kuidhinisha mkataba wa kupiga marufuku majaribio ya nuklia

UN unayahimiza mataifa yote kuidhinisha mkataba wa kupiga marufuku majaribio ya nuklia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anayahimiza mataifa yote ambayo hayajaidhinisha mkataba wa kupiga marufuku majaribiyo ya nuklia kufanya hivyo kwa haraka.

Katika ujumbe wake kuadhimisha siku ya kwanza ya kimataifa dhidi ya majaribio ya nuklia itakayo sherehekewa Jumapili, Bw Ban alisisitiza kwamba inawezekana kuwepo na dunia isiyo na silaha za nuklia, na kwamba kumekuwepo na maendeleo muhimu mnamo 2010.

Katibu mkuu alisema anategemea kufanya kazi pamoja na washirika wote kupunguza matumuizi ya mipango ya nuklia na kuondowa kabisa kitisho cha nuklia duniani. Nguzo muhimu ya mkakati huo ni mkataba jumla wa kupiga marufuku majaribio ya nuklia.

Siku ya kimataifa ya kupiga marufuku majaribio ya silaha iliidhinishwa na Baraza Kuu mwezi Januari ili kuhamasisha watu kufahama na kuelewa juu ya athari za miripuko ya majaribio ya silaha za nuklia au miripuko mingine yeyote ya nuklia na haja ya kukomesha hali hiyo ni njia moja ya kufikia lengo la kuwepo na dunia isiyo na silaha za nuklia.