Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la wataalam la Umoja wa Mataifa kuhusu uvamizi wa meli na wanajeshi wa Israel lakamilisha ziara yake nchini Uturuki

Kundi la wataalam la Umoja wa Mataifa kuhusu uvamizi wa meli na wanajeshi wa Israel lakamilisha ziara yake nchini Uturuki

Kamati huru ya kimataifa ya wataalamu iliyoteuliwa na rais wa baraza linalohusika na haki za kibinadamu kuchunguza uvamizi kwenye msafara wa meli uliokuwa ukielekea ukanda wa Gaza imekamilisha ziara yake ya wiki moja nchini Uturuki.

Wakati wa ziara hiyo wataalamu hao waliwahoji mashahidi na maafisa wa serikali waliolezea kuhusu tukio hilo lililojiri tarehe 31 mwezi Mei mwaka huu ambapo pia waliendesha ukaguzi kwenye meli hiyo iliyovamiwa na wanajeshi wa Israel. Wataalamu hao pia wanatarajiwa kuanza ziara yao nchini Jordan na nchi majirani kati ya tarehe 29 mwezi huu na tarehe 4 mwezi ujao kuwahoji mashahidi kutokana na tukio hilo.

Wataalamu hao wanawajumuisha jaji wa zamani wa mahakamu ya kimataifa ya uhalifu ICC K. Hudson-Phillips , Sir Desmond de Silva mwendesha mashtaka wa zamani wa mahakama ya ICC kuhusu uhalifu wa kivita nchini Sierra Leone na Bi Shanthi Dairiam mtaalamu wa masula ya haki za binadamu kutoka Malaysia