Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi wa wakimbizi 100,000 kutoka Afghanistan warejea nyumbani mwaka huu

Zaidi wa wakimbizi 100,000 kutoka Afghanistan warejea nyumbani mwaka huu

Idadi ya wakimbizi wa Afghanistan wanaorejea makwao kutoka Pakistan na Iran imepanda na kufikisha wakimbizi 100,000 mwaka huu ikiwa ni mara mbili zaidi ya mwaka uliopita kulinganana ripoti ya umoja wa mataifa.

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la umoja wa mataifa UNHCR linasema kati ya wakimbizi hao wanaorejea nyumbani 95,000 wanatoka nchini Pakistan. Wanaorejea makwaa wanadai kuwa wamelazimika kurudi nyumbani kutokana na ugumu wa maisha nchini Pakistan na kuimarika kwa usalama katika baadhi ya maeneo nchini Afghanistan. Hata hivyo idadi ya wakimbizi wanaorejea makwao huwa ni tofauti kila mwaka baada ya wakimzi 54,000 tu kurejea nyumbani mwaka uliopita ikilinganishwa na wakimbizi 278,000 waliorejea nyumbani mwaka 2008.