Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikosi cha UNAMID na serikali ya Sudan waafikiana kuimarisha usalama katika jimbo la Darfur

Kikosi cha UNAMID na serikali ya Sudan waafikiana kuimarisha usalama katika jimbo la Darfur

Kikosi cha pamoja cha umoja wa mataifa na muungano wa Afrika UNAMID pamoja na serikali ya Sudan wameafikiana kushirikiana kuimarisha usalama kwenye jimbo lilalokabiliwa na mzozoz la Darfur nchini Sudan.

Makubaliano hayo yaliafikiwa kwenye mkutano kuhusu kupatikana kwa amani kwenye jimbo la Darfur uliondaliwa Khartoum mji mkuu wa Sudan na kuhudhuiriwa na mkuu wa kikosi cha UNAMID Professor Ibrahim Gambari, rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo Mbeki ambaye ni mwenykiti wa kamati kuu ya muungano wa Afrika pamoja na mjumbe maalum wa Marekani nchini Sudan Scott Gration.

Wote hao waliafikia uamuzi wa kuwepo kwa ushirikiano kati ya vikosi vya UNAMID na serikali ya Sudan kuleta utulivu katika jimbo la Darfur nia pia kuwepo kwa maendeleo. Professor Gambari amesema kuwa ataunga mko ushirikiano kati ya UNAMID, polisi na jeshi la sudan kuhakikisha kuwa kuwepo kwa usalama kwenye jimbo la Darfur.