Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna wa Haki za Binadamu UM alaani vikali mauwaji ya wahamiaji 72 chini Mexico

Kamishna wa Haki za Binadamu UM alaani vikali mauwaji ya wahamiaji 72 chini Mexico

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya Haki za Binadamu Navi Pillay ameelezea masikitiko yake kutokana na mauwaji ya wahamiaji 72 nchini Mexico yaliyofanywa katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo.

Kamishna huyo amelaani hatu hiyo na kusema kuwa inasikitisha kuona umati mkubwa wa watu wakipoteza maisha. Ameongeza kuwa hali hiyo inaelezea namna ambavyo tatizo la wahamiaji lilivyo tete katika eneo hilo.

Maafisa wa serikali nchini humo walikuta mrundikano wa maiti iliyokuwa na watu 72, ikiwemo wanawake 14 ambao wanaaminika waliuwawa na kundi fulani la wahalifu.Wahanga hao wanaarifiwa kuwa ni wahamiaji wanaotoka Kusin na Kaskazini mwa Amerika.

Kamishna huyo amesema kuwa bado anaimani na serikali ya Mexico namna inavyopigana kutokomeza vitendo vya kihalifu lakini amasisitiza kuwa lazima waliohusika kwenye mauwaji hayo waletwe kwenye mkondo wa dola.