Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu milioni 1.3 hufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani : UNECE

Watu milioni 1.3 hufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani : UNECE

Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Ulaya, UNECE pamoja na shirikisho la kimataifa la mpira wa vikapu FIBA, zimezindua Alhamisi kampeni mpya ya kupasha habari juu ya usalama barabarani wakati sambamba na kufunguliwa kwa mashindano ya Mpira wa vikapu duniani yanayoanza Uturuki kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 12.

Kaulu mbiyo ya kampeni hiyo ni "tunacheza na kuendesha kwa kufuata kanuni," na imetayarishwa kwa lengo la kuwapasha habari watu wote duniani hasa vijana ambao ni mashabiki au wachezaji wenyewe pamoja na kuhamasisha watu kuheshimu kanuni za barabarani pamoja na zile za uwanjani.

Akizindua kampeni hiyo Katibu Mtendaji wa UNECE, Jan Kubis alisema "Kila mwaka takriban watu milioni 1.3 wanafariki kutokana na ajali za barabarani. Hii inamaanisha kiasi ya vifo 3,500 kila siku. Hali aibadiliki kua nzuri badala yake katika sehemu nyingi za dunia kwa sababu, kwa mfano magari zaidi yanatumika barabarani na hapo ajali zinaongezeka".

Bw Kubis alisema kuongezeka kwa idadi ya wakazi duniani inachangia pia kwa namna fulani changamoto hii, kwa vile vijana wengi zaidi wanafika umri wa kuendesha magari na mara nyingi bila kufuata kanuni za barabarani.