Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapinduzi ya kilimo Afrika yanahitaji juhudi za dhati za kila mtu UN

Mapinduzi ya kilimo Afrika yanahitaji juhudi za dhati za kila mtu UN

Mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa cha maendeleo ya mashambani, Kanayo Nwanze, amesisitiza haja ya hii leo ya kuwepo na sera kabambe, uwezo wa kufika katika masoko, miundo mbinu na teknolojia za bei nafuu ili kuhakikisha usalama wa chakula barani Afrika.

Akizungumza kabla ya kufunguliwa kwa mkutano muhimu juu ya kilimo barani Afrika mwezi ujao Bw Nwanze ambae ni rais wa idara ya kimataifa kwa ajli ya maendeleo ya kilimo IFAD, alisema mapinduzi ya kilimo yatakayoweza kudumu na kuhusisha wote ni yale yatakayoongozwa na mapinduzi ya sera ambapo serikali inachukua jukumu la uwongozi.

Bw Nwanze atachukua ujumbe huo na kufikisha kwenye Jopo la Mapinduzi ya Kijani Afrika AGRF linalodhaminiwa na Mungano kwajili ya Mapinduzi ya kijani Afrika kwajili ya Afrika litakalofanyika Accra Ghana kuanzia Septemba 2.

Wakati wa mkutano huo Bw Nwanze alisisitiza juu ya kile kinachohitajika kwajili ya mapindnzi mengine ya kilimo Afrika ikiwa ni pamoja na uwezo wa kufika kwenye masoko, ardhi na miundo mbinu pamoja na teknolojia mpya kwajili ya watu wa maeneo ya mashambani.

Mkutano huo wa wiki ijayo huko Accra Ghana, utakao hudhuriwa na viongozi, wakulima, taasisi za kifedha na mashirika yasiyo ya kiserikali utanongozwa kwa pamoja na Rais John Atta Mills wa Ghana na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan na unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika.