Skip to main content

Rais wa Brazil ajiunga na kampeni ya FAO ya kupambana na njaa duniani

Rais wa Brazil ajiunga na kampeni ya FAO ya kupambana na njaa duniani

Rais Luiz Lula da Silva wa Brazil amejiunga na kampeni ya kimataifa ya kupambana na njaa iliyotayarishwa na idara ya Chakula na Kilimo FAO, kwa kutiasini jina lake kwenye waraka ya kimataifa ya FAO ya kupambana na njaa iliyopewa jina la "bilioni1njaa" na akapuliza firimbi manjano ya kampeni hiyo iliyopewa jina la " firimbi dhidi ya njaa".

Sherehe za kupuliza firimbi zilifanyika Brasila mji mkuu wa Brazil hii leo Alhamisi. Karibu nusu milioni ya watu kote duniani wameshatia saini waraka huo wa FAO "bilioni moja njaa" unaotoa wito kwa viongozi wa dunia kuzifanya juhudi za kukomesha njaa kua kipau mbele chao cha juu. Waungaji mkono wa kampeni wanaombwa kupuliza firimbi dhidi ya njaa.

Lengo la FAO ni kutaka kupata watu milioni moja kutia saini waraka huo ifikapo mwisho wa Novemba na kuwasilisha kwa mataifa wanachama 192 yanayotarajia kuhudhuria baraza la utawala la FAO. Takriban watu bilioni moja duniani kwa wakati huu wanataabika na hali sugu ya njaa.

"Njaa inaumiza na inauwa. Na hatuwezi kubaki bila kujali tukiwa tunakabiliwa na machungu kama haya", alisema mwakilishi wa FAO nchini Brazil Helder Mutela wakati wa sherehe za huko Brasilia. Rais Lula da Silva alipuliza firimbi kabla ya kumalizika kwa sherehe hizo.

Unaweza kutia saini waraka wa "bilioni1njaa" kwenye ukurasa wa tovuti http://www.1billionhungry.org/