Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuia ya Kimataifa imelaani al-Shabab kwa mashambulizi dhidi ya raia wa Somalia

Jumuia ya Kimataifa imelaani al-Shabab kwa mashambulizi dhidi ya raia wa Somalia

Norway, Marekani ofisi ya Umoja wa Afrika huko Somalia Umoja wa Ulaya, IGAD, Umoja wa nchi za Kiarabu, pamoja na ofisi ya masuala ya kisiasa ya Umoja wa Mataifa kwajili ya Somalia, zimetoa taarifa ya pamoja Alhamisi kulaani vikali mashambulizi yanayoendelea dhidi ya wakazi wa Mogadishu, yanayofanywa na wanaharakati wenye siasa kali wa kundi la al-Shabab.

Taarifa hiyo imtoa pia risala za rambiambi kwa wote wanaotabika kote nchini Somalia na hasa kwa familia za walouwawa huko Mogadishu. Taarifa imesema utaratibu wa amani utaendelea na kuahidi kuunga mkono juhudi za serikali ya Somalia na wananchi wa Somalia katika kazi yao ya kukomesha mapigano na kupatikana matumaini yenye mustakbal mzuri.