Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN inaimarisha huduma Pakistan wakati mafuriko yawaathiri watu 17

UN inaimarisha huduma Pakistan wakati mafuriko yawaathiri watu 17

Umoja wa Mataifa umeimarisha juhudi zake za huduma za dharura huko Pakistan wakati idadi ya wanaoathirika na janga hilo mbaya imefikia watu milioni 17.

Idara ya huduma za dharura ya Umoja wa Mataifa OCHA, imesema kwamba msaada wa dharura unahitaji kuongezwa katika majimbo ya Sindh na Punjab, kutokana na kufurika maeneo mepya huko Sindh ya kusini katika siku za hivi karibuni.

Msemaji wa OCHA huko Pakistan, Stacey Winston akizungumza na Derrick Mbatha wa radio ya Umoja wa Mataifa anasema hali ni ya wasi wasi huko maeneo ya kusini.

"Tuna wasi wasi sana kutokana na kuendelea kwa mafuriko yanayosababisha watu zaidi kukimbia makazi yao na uwezekano wa magonjwa kuzuka pamoja na ukosefu wa maji masafi na shirika la Afya Duniani, WHO limefungua zahanati za kutibu watu wanaoharisha kwa sababu watoto na watu wazee pamoja na wanawake wajawazito wako hatarini zaidi kuambukizwa na magonjwa yanayotokana na maji."

OCHA inasema juhudi za kuwasilisha vifaa na kurahisisha usafiri hadi maeneo ambayo watu wamekwama kutokana na mafuriko zimeimarishwa na kwamba vyombo vya kusafirisha msaada kwa anga vinahitajika haraka.