Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yaridhishwa na Serikali ya Angola namna inavyokabiliana kupunguza vifo vya kina mama na watoto

UNICEF yaridhishwa na Serikali ya Angola namna inavyokabiliana kupunguza vifo vya kina mama na watoto

Kwa mara ya kwanza Serikali ya Angola imepiga hatua kubwa katika kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wadogo.

Hata hivyo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limesema kuwa bado nchi hiyo inakabiliwa na mazingira hatarishi juu ya kina mama wajawazito na watoto.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Angola Dr. Koen Vanormelingen amesema kuwa bado familia nyingi maskini hasa zile zinazoishi vijijini hazijafikiwa kikamilifu na huduma za kiafya, hatua ambayo inaongeza hali ya hatari kwa siku za mbeleni.

Serikali ya Angola hivi karibuni ilizindua kampeni maalumu inayozingatia upunguzaji wa vifo kwa kina mama wajawazito na watoto. UNICEF imekaribisha hatua hiyo ikisema kuwa itafungua ukurasa mpya kwa kuziwezesha familia nyingi kufikiwa na huduma za afya