Serikali, mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali washirikiana kulinda maeneo yenye utajiri wa viumbe Amerika ya kusini

26 Agosti 2010

Amerika ya kusini pamoja na nchi za Caribbean yametajwa kama maeneo yaliyo na utajiri wa sehemu nyingi za kiasili na kibaolojia duniani huku nchi za Brazil, Colombia, Equador, Mexico, Peru na Venezuela zikitajwa kuwa na kati ya asilimia 60 na 70 ya aina ya viumbe duniani.

Kama moja ya njia ya kutatua tatizo hilo shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na lile linalohusika na uhamaji wa viumbe CMS yaliwaleta pamoja mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutoka nchi 17 za Amerika ya kusini na nchi za Caribbean kwenye warsha kwenye mji wa Panama kujadili njia za kukabiliana na hali hiyo. Mkutano huo uliofanyika kati ya tarehe 23 na 25 mwezi huu ulitumika kutoa mafunzo jinsi ya kutekeleza njia za kulinda maeneo hayo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter