Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikosi cha UM Lebanon kimetoa msaada wa magari kwa jeshi la nchi hiyo

Kikosi cha UM Lebanon kimetoa msaada wa magari kwa jeshi la nchi hiyo

Kikosi cha mpito cha Umoja wa mataifa huko Lebanon, UNIFIL kimelikabidhi jeshi la Lebanon magari 39 katika juhudi za kuongeza uwezo wao wa kuimarisha usalama huko kusini mwa nchi.

Katika sherehe za kukabidhi magari hayo kwenye makao makuu ya UNIFIL Naqoura, kamanda wa kikosi hicho Meja Jenerali Alberto Asarta Cuevas alisisitiza kwamba hali imeboreka sana nchini na ushirikiano kati ya UNIFIL na jeshi la Lebanon umekua msingi wa kutekeleza mamlaka yao.

Alisema, mkakati wa kuondoka kwa UNIFIL unaambatana na uwezo wa jeshi la Lebanon kuhakikisha utulivu huko Lebanon ya kusini.